WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa amepata udhamini wa kishindo katika mkutano uliofanyika jana katika ofisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni.
Lowassa alipata udhamini huo baada ya wanachama kujitokeza katika ofisi za Makao Makuu ya CCM ya Wilaya ya Kinondoni, Mkwajuni, Dar, ambapo alipata zaidi ya wadhamini 212,150 huku akisema Dar imevunja rekodi ya mikoa yote ya Tanzania.
Akizungumza na maelfu ya wananchi waliofika katika mkutano huo Lowassa alisema kuwa amefurahishwa na watu waliojitokeza kumdhamini kwa kishindo kikubwa na hivyo hatavunjwa moyo na maneno ya watu yanayovumishwa kuwa anawapatia fedha ili wafike kwenye mkutano wake .
Lowassa aliongeza kuwa anawaomba Watanzania wampe ridhaa ya kuwa rais wao kwani atahakikisha mianya yote ya rushwa na utendaji mbovu wa kusuasua anausimamia kwa haki na weredi na ndani ya miezi sita tayari matokeo yatakuwa yameonekana.
“Nawaombeni wananchi mnipeni ridhaa ya kuingia ikulu yaani nitahakikisha mianya yote ya rushwa na ufisadi nautokomeza, muyapuuze maneno na minong’ono ya watu kutaka kunichafua,” alisema.
Mwanasiasa Mkongwe hapa nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akisani fomu ya udhamini mbele ya Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono mgombea huyo.
Zoezi hili lilifanyika jana jioni ya Juni 27, 2015 kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni, Mkwajuni Jijini Dar ambapo Lowassa alipata jumla ya Wadhamni 212, 150 na kuifanya Dar es salaam kuwa Mkoa wa kwanza kuwa na idadi kubwa ya WanaCCM waliomdhamini