Mimba ya muigizaji Aunt Ezekiel imeanza kumtibua baada ya nyota huyo
kushindwa kufanya baadhi ya kazi ambazo alikuwa akizifanya mwenyewe.
Kwa mujibu wa chanzo cha GPL, kutokana na tumbo kuwa kubwa, Aunt kwa
sasa hawezi kufunga viatu vyake, kufua, kuosha vyombo na hata akitaka
kwenda toileti inabidi apewe kampani na mtu.
“Mh! Jamani Aunt hata kuinama ni mtihani sasa sijui kama ni kujidekeza
au nini maana anapokuwa karibu na bebi wake ndiyo usiseme ni full kudeka
anasema akiinama anaumia jamani?“Eti sasa hivi shosti wake Wema Sepetu
na bebi wake Mose Iyobo ndiyo wamekuwa wakifanya kazi ya ziada kumsaidia
kila kazi nyingi anazoshindwa,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya chanzo hicho kupenyeza habari, paparazi wa GPL alimsaka Aunt
na kufanikiwa kumnasa kwa nyakati tofauti akiwa anasaidiwa kufungwa
viatu na Wema pamoja na Iyobo.Alipoulizwa Aunt kama anashindwa kweli
kufanya kazi mwenyewe au anadeka, alifunguka:
“Jamani hivi niiname nimkunje mtoto wangu bila sababu za msingi na watu
wapo ambao wanaweza kunisaidia kwa nini nijiumize, acheni nisaidiwe,”
alisema Aunt.Kwa upande wake, Mose ambaye inaaminika kuwa ndiye mhusika
wa mimba hiyo ya Aunt alipozungumza na mwanahabari wetu, alijisifu na
kusema anafurahi kuwa baba bora wa Aunt.
“Sioni tatizo kutamka, mimi ndiye mhusika mwenyewe, baba bora mimi,
watakaochukia wachukie,” alisema Iyobo.Kabla ya kuanzisha uhusiano na
Iyobo, Aunt aliolewa na mfanyabiashara, Sunday Demonte anayedaiwa
kufungwa nchini China kwa msala wa madawa ya kulevya.
Home »
BURUDANI
,
UDAKU
» MAHABA ,MAHABANI..MIMBA YA AUNT EZEKIEL YAMFANYA ASHINDWE KUVAA VIATU MWENYEWE!!
MAHABA ,MAHABANI..MIMBA YA AUNT EZEKIEL YAMFANYA ASHINDWE KUVAA VIATU MWENYEWE!!
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website