STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper
ameamua kumuweka bayana mchumba wake wa sasa anayejulikana kwa jina la
G. Modo baada ya kukaa kimya muda mrefu tangu alipoachana na Abdallah
Mtoro ‘Dallas’.
Akizungumza na gazeti hili hivi
karibuni, Wolper alisema alikuwa kimya kwa muda mrefu kwa ajili ya
kutafakari kwanza maana asingeweza kukurupuka wakati bado
hawajachunguzana tabia vizuri na mpenzi wake huyo.
“Kiukweli nafurahia sana uhusiano
wangu wa sasa na siwezi kusema moja kwa moja kuwa ndiye mume wangu kwa
vile najua kila kitu kinaongozwa na Mungu, ninachokiomba ni ndoto yangu
ikamilike tu kwani nahisi niliyempata ni sahihi kwangu,” alisema Wolper.
Wolper aliongeza kuwa kama siku Mungu
atajalia kwa mpenzi wake huyu kitakachofuatia ni kwenda moja kwa moja
kwa wazazi wa pande zote mbili ili kupata baraka na ndiyo kitu ambacho
anakiomba kila kukicha
--GPL--
BAADA YA KIMYA CHA MUDA MREFU, JACKLINE WOLPER AMWANIKA MPENZI WAKE MPYA HADHARANI
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website