MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, leo anatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara utakaofanyika viwanja vya Malimbe, katika maeneo ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), jijini Mwanza.
Mkutano huo ni mwendelezo wa harakati za kujenga na kuimarisha chama,
ambapo Katibu Mkuu wa CHADEMA taifa, Dk. Willibrod Slaa kwa sasa yupo
katika ziara kama hiyo katika mikoa ya Tabora, Singida, Kigoma na
Shinyanga.
Akizungumzia ujio wa Mbowe, jijini Mwanza jana, Ofisa Operesheni wa
CHADEMA Kanda ya Ziwa Magharibi, Tungaraza Njugu alisema kiongozi huyo
wa taifa pamoja na viongozi wengine watazungumzia mambo mbalimbali
muhimu kwa ustawi wa taifa.
“Mwenyekiti wetu CHADEMA taifa, Freeman Mbowe yupo Mwanza na leo
atahutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Malimbe kule SAUT.
Lengo la ziara hii ni kuimarisha na kujenga chama kwa misingi ya
uwajibikaji,” alisema.
Aliongeza kuwa Mbowe jana alifungua Mkoa wa Vyuo Vikuu vilivyopo
mkoani Mwanza kwa lengo la kuthamini uwepo wa wasomi katika harakati za
kuijenga Tanzania na kutafuta usawa kwa jamii.
Alisema katika mkutano huo Mbowe alisema CHADEMA inatarajia kuandaa
kitabu, kuelezea chama hicho kilikotoka na kilipo sasa, ikiwa ni moja ya
kuwaenzi waasisi wake