Maombi ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa
Ponda ya kuomba ufutiwa shtaka la kukiuka uamuzi wa mahakama, yamebaki
njiapanda baada ya Jamhuri kuyawekea pingamizi la kisheria, ikiiomba
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iyatupilie mbali.
Wakili
Mkuu wa Serikali, Bernard Kongola alidai hayo jana mbele ya Jaji Rose
Temba kabla ombi hilo halijaanza kusikilizwa. Katika ombi hilo, Shekhe
Ponda anaiomba Mahakama ifanye marejeo ya uamuzi wa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Morogoro, uliokataa kumfutia mashitaka ya kukiuka amri ya
Mahakama.
Akiwasilisha
hoja zake, Wakili Kongola alidai ombi hilo ni batili kwa kuwa kiapo
kinachounga mkono kina mapungufu, kinyume na Kifungu cha 8 cha Sheria ya
Viapo.
Alidai
kuwa upungufu huo ni kutokuwepo kwa tarehe katika kiapo hicho,
kilichoapwa na Wakili Hamidu Ubaidi. Pia, alidai kiapo hicho hakijaeleza
kama aliyeapa, alifanya hivyo mbele ya wakili anayemfahamu.
Alidai
upungufu huo hauwezi kurekebishwa, hivyo ni kama hakijawasilishwa na
kuiomba Mahakama ione ombi hilo ni batili na halijawasilishwa kwa mujibu
wa sheria.
Wakili
wa Ponda, Nassoro Juma aliomba Mahakama itupilie mbali pingamizi hilo
kwa kuwa halina msingi kisheria, bali ni maelezo, na kuangalia ombi hilo
kwa jicho la haki na siyo kiufundi.
Aidha,
alidai pingamizi hilo limewasilishwa kwa nia ya kuchelewesha kesi ili
mshitakiwa aendelee kukaa rumande na kesi inayomkabili, isiendelee.
Alidai
kuwa hakuna upungufu wowote katika kiapo hicho, kwa kuwa kinaonesha
kilichukuliwa Oktoba 8, mwaka huu na ombi hilo liliwasilisha Oktoba 10,
mwaka huu.
Alidai
kiapo kilichowasilishwa, kina tarehe na wakili aliyeapa alifanya hivyo
mbele ya Wakili anayemfahamu na inawezekana katika nakala za upande wa
Jamhuri, inaonekana kina upungufu, lakini Mahakama inaongozwa na nyaraka
zilizo kwenye kumbukumbu za mashauri.
Jaji
Temba aliahirisha shauri hilo hadi Desemba 11, mwaka huu, atakapotoa
uamuzi wa kusikiliza au kutupilia mbali ombi hilo. Ponda anadaiwa
kukiuka amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyomtaka kutotenda
kosa kwa mwaka mmoja, na kutotoka nje ya Mkoa wa Dar es Salaam bila
kibali cha Mahakama.
Hata
hivyo, Shekhe Ponda aliomba mashitaka hayo yafutwe katika Mahakama ya
Morogoro au yahamishiwe katika Mahakama iliyotoa amri hiyo, kwa kuwa
Mahakama hiyo ya Morogoro haina mamlaka ya kusikiliza