Home » » APOKEA KICHAPO BAADA YA KUFUMANIWA NA ''DEM'' WA RAFIKI YAKE KISA...''MTOTO KAJALIWA MZIGO''

APOKEA KICHAPO BAADA YA KUFUMANIWA NA ''DEM'' WA RAFIKI YAKE KISA...''MTOTO KAJALIWA MZIGO''

 Katika hali ya kustaajabisha na pengine ikaingia kwenye kumbukumbu ya maisha yake, mtu mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Sebastiani mkazi wa Nkuhungu jijini Dooma, juzi Jumapili alijikuta kwenye aibu kubwa baada ya kufumaniwa na mchumba wa swahiba yake wa kufa na kuzikana.

Tukio hilo ambalo lilitokea mishale ya saa 3 usiku kwenye gesti ya Las Vegas iliyopo maeneo ya Area C jijini Dodoma, ilitokana na mchumba wa jamaa (binti) kumtonya jamaa yake kwamba kuna mtu anamtaka kimapenzi.

"Baada ya mchumba angu kuniambia hayo niliangalia ile namba na kugundua mtu aliyekuwa kimtaka mchumba wangu ni rafiki yangu wa zamani sana tena ni wakufa na kuzikana," alisema jamaa huyo kwa masikitiko. Alisema kutokana na jamaa huyo kutaka kutembea na mchumba wake na yeye aliamua kumfanyia umafia wa kumuumbua mbele ya jamii ili iwe fundisho kwa wengine.

"Nilikaa nikatafakari sana maana jamaa alikuwa akimtumia mchumbaangu meseji ambazo siwezi kuzisoma hapa maana ni aibu lakini kubwa alikuwa akimtaka mchumba wangu kinyume na maumbile akidai amejaaliwa sana," alieleza jamaa huyo mbele ya umati wa watu waliojitokeza kushuhudia tukio hilo.

Taarifa zinaeleza kwamba baada ya hapo mipango ya kumfumania jaama huyo ilianza kuandaliwa na takribani mara mbili walipopanga kukutana na mchumba huyo wa mtu alichomoa kwa madai kwamba alikuwa akizidiwa na kazi.

"Kama mara mbili walipanga kukutana lakini dakika za mwisho jamaa alichomoa kwa madai ya kuzidiwa na kazi lakini leo za mwizi zimetimia," alidai jamaa huyo baada ya kumfumania rafiki yake huyo akiwa uchi wa mnyama na mchumba wake kwenye gesti hiyo chumba namba A12. Dakika chache baadae alifika mkewe wa mfumaniwa na kutokana na tukio hilo alisema hana la kusema zaidi ya kumshukuru mungu kwa aibu aliyoipata toka kwa mumewe huyo wa ndoa.

"Kiukweli sina la kusema hii ni aibu kubwa sana...mume wangu kila siku anadai hapa pesa za matumizi nauza mkaa ndio tule na watoto kumbe ndio mambo aliyokuwa anayafanya, nashukuru sana," alisema mke huyo mbele ya waandishi wa habari.

Hadi mwandishi wetu anaondoka eneo la tukio, aliwaacha wakiwa ndani ya chumba wakiendelea kupata kichapo...
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
 
Copyright © 2011. PERUZI HABARI - All Rights Reserved
Proudly powered by Peruzitz