STAA wa filamu Bongo, Wema Sepetu amefungukia ugomvi ambao hutokea mara
kwa mara na shosti wake ambaye pia ni muigizaji, Aunt Ezekiel
usiingiliwe na mtu kwani wanapogombana tofauti zao wanazimaliza wenyewe
na si mtu mwingine yeyote.
Akizungumza na Amani Wema alisema kuwa, yeye na Aunt ni watu waliopo
karibu sana na wanaopendana hivyo inapotokea wanagombana huwa ni kitu
kidogo kwao kwani huyamaliza na maisha yanaendelea kama kawaida.
“Jamani nyinyi mtuache tu, tunatibuana na Aunt, tunajuana vizuri sana
ugomvi wetu ni wa mara kwa mara lakini tunamalizana wenyewe kwa sababu
ukweli ni kwamba hatuwezi kukaa mbalimbali kwa muda mrefu kutokana na
kupendana,” alisema Wema.
Wema Sepetu Afungukia Ugomvi Wake na Aunt Ezekiel
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website