Video ya aibu inayomuonesha msanii maarufu wa filamu Bongo, Wema Sepetu
‘Madam’ akicheza kihasara mbele ya mwanaume imevuja, Risasi Jumamosi
linayo kibindoni.
‘Klipu’ hiyo ambayo Wema anaonekana akikata mauno huku suruali aliyokuwa
amevaa ikimvuka na kuacha wazi sehemu ya makalio yake, ilivujishwa hivi
karibuni na mdau mmoja wa burudani ambaye hakupenda jina lake liandikwe
gazetini.
“Hii video niliichukua siku ya ile eventi ya Christian Bella ya kutimiza
miaka 10 pale Escape One. Wakati akicheza na msanii wa Kundi la Pah One
aitwaye Igwe, Wema alionekana kama alikuwa amelewa, alikuwa akikata
mauno lakini aibu zaidi ilikuwa pale ambapo ile suruali yake ilipomvuka
na sehemu ya makalio yake kubaki wazi.
“Sidhani kama alikuwa kavaa kufuli, baadhi ya watu waliokuwa
wakimkodolea macho walishindwa kuamini kama ni Wema yule wanayemjua,”
alisema mnyetishaji huyo.
Baada ya mwandishi wetu kupata nafasi ya kuiangalia mwanzo mpaka mwisho,
alijiridhisha kuwa aliyekuwa akionekana kwenye video hiyo ni Wema na
kweli alichokuwa akifanya ni aibu tupu.
Aibu yake ni pale ambapo suruali inamvuka na kuacha sehemu zake za siri
wazi lakini pia staili ya kumkatikia msanii aliyekuwa akicheza naye
kwani jamaa alikuwa ‘akikamatia chini’ huku naye akionekana kutokwa na
udenda.
Paparazi wetu alijaribu kumtafuta Wema ili kuizungumzia ‘klipu’ hiyo lakini simu yake kila ilipopigwa ilikuwa haipokelewi.
Chanzo:GPL
Video ya Aibu ya Wema Sepetu Yavuja!
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website