Jike Shupa na Nuh mziwanda |
Akizungumza katika mahojiano rasmi, msichana huyo alisema hapendi na anakasirishwa sana kuona watu wakimfananisha na staa huyo wa muziki, akidai hafanani naye kwani yeye ni mzuri na msafi, licha ya kuwa alianza zamani kuwa staa katika Bongo Fleva.
“Mimi nilianza ku-shine zamani sana katika video za Bongo Fleva, enzi hizo, nimecheza video ya Daz Baba ya Mrembo namba Nane, au Juma Nature nimecheza video yake, hivi yeye na Nature nani staa? Mimi nitafute kiki kwa Shilole, looh, mimi nilichofanya nimefanya kazi, nimelipwa vizuri basi,” alisema.
Alimtupia vijembe mwimbaji huyo kwa kusema alimuona wakati akija mjini akitokea Igunga, kwa hiyo hamtishi kwa lolote, kwani kama ni maisha anaishi kwa shughuli zake za kisanaa na hana matatizo na mtu.
Ili kuweka uzani wa habari hiyo, gazeti hili lilimtafuta Shilole na kumwelezea kinagaubaga juu ya madai ya Jike Shupa ambapo nyota huyo wa Wimbo wa Paka la Baa akafunguka;
“Mimi ni staa mkubwa sana kwa huyo mtu, mwambie asitafute kiki kupitia jina langu, kwanza huu ni Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, sina muda wa kujibishana na mtu kama huyo,” alisema kwa kifupi.
Wawili hao wameingia katika uhasama, baada ya Zena ambaye pia hujiita Zuu, kuigiza kama Shilole katika Wimbo wa Jike Shupa wa Nuh, ambao ni kama umezu-ngumzia maisha yake ya kimapenzi na Shilole, aliyoishi kwa kupigwa, kusimangwa na kunyanyaswa!