Home » , » Auawa na Mdogo wake Baada ya Kumfumania Akifanya Mapenzi na Mkewe

Auawa na Mdogo wake Baada ya Kumfumania Akifanya Mapenzi na Mkewe

Mkazi wa Mahembo Manyanda Manyilizu (40) ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mdogo wake baada ya kumfumania akiwa na mkewe.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Dismas Kisusi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi katika Kijiji cha Mawemilu.

“Manyilizu alimkuta mdogo wake akifanya mapenzi na mkewe, alivyomuhoji, mdogo wake alichukua kitu akampiga nacho kichwani hivyo alifariki dunia wakati akiendelea na matibabu katika zahanati ya Kijiji cha Mawemilu,” alisema Kisusi.

Alidai mtuhumiwa na mwanamke walikimbia baada ya kufanya tukio hilo.

Katika tukio jingine, watu wawili wameuawa kwa kupigwa mawe na marungu kisha miili yao kuchomwa moto na wananchi.

Kisusi alisema tukio hilo lilitokea juzi katika Kijiji cha Shimba wilayani Kahama.

Kisusi alisema watu hao walituhumiwa kuwa ni majambazi baada ya kumvamia Mchongaraji Ndalawa (65), akiwa amelala nyumbani kwake wakimtaka awape fedha.

“Alivyosema hana walimkata kwa panga kichwani, ndipo wananchi walijichukulia sheria mkononi kwa kuwaua,” alisema.

Majeruhi huyo amelazwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama na hali yake inaendelea vizur
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
 
Copyright © 2011. PERUZI HABARI - All Rights Reserved
Proudly powered by Peruzitz