Diwani Baba Levo Akibambia Mtoto |
SIKU YA TUKIO
Tukio hilo la aina yake lilitokea usiku wa kuamkia Desemba 29, Mwaka huu Kijitonyama jijini Dar, ambapo wawili hao walikuwa wamehudhuria kwenye bonge la pati lililokuwa limeandaliwa na msanii mwenzao Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
NI PATI YA KUACHANA
Shilole aliandaa sherehe hiyo maalum kwa lengo la kufurahi pamoja wakati akijipongeza baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.
BABA LEVO NDIYE MC
Wakiwa kwenye sherehe hiyo, Baba Levo alikabidhiwa jukumu la kuwa mshehereshaji (MC) wa pati hiyo, ambapo alianza kwa kuwakaribisha wageni wote waalikwa kisha kuianza sherehe rasmi.
MTUNGI MDOGOMDOGO
Kama ilivyo ada ya watoto wa mjini wanavyosema sherehe hainogi bila ‘maji ya Ilala’, Baba Levo aliungana na wageni waalikwa kuanza kupiga ‘maji matamu’ taratibu huku wakionekana kuchangamka kadiri muda ulivyozidi kuyoyoma.
LINAH AANZA KUCHANGAMKA
Linah ndiye aliyekuwa wa kwanza kuonesha kwamba ‘mambo’ yamepanda kichwani baada ya kuinuka mahali alipokuwa amekaa na kuanza kucheza muziki huku akirusha miguu kama ile staili ya Mapanga Shaa ya Wanaume Halisi.
IMG_8730
Mastaa kibao walikuwepo kwenye pati hiyo.
UVUMILIVU WAMSHINDA MH. DIWANI
Mheshimiwa diwani huyo mwenye mbwembwe na maneno mengimengi ya kufurahisha, naye uvumilivu ulimshinda ambapo alijikuta akiinuka na kuanza kucheza peke yake huku akionekana kumkodolea macho zaidi Linah ambaye wakati huo alikuwa amezidisha mbwembwe.
KABAAAH! AMBAMBIA
Huku na huku haikupita muda mrefu sana, Baba Levo alijikuta tayari yupo kwenye mgongo wa Linah na kuanza kucheza naye huku mrembo huyo akimpa ushirikiano kama anayesema: “Ulikuwa wapi muda wote nateseka kwa kucheza peke yangu.”
WAALIKWA FULL KUSHANGALIA
Kutokana na waalikwa wengi kuwa tayari ‘wameshapendeza’, kadiri Baba Levo na Linah walivyokuwa wakicheza kwa staili ya kukata mauno huku mheshimiwa huyo akiwa amemkumbatia vilivyo Linah, waalikwa walishangilia kwelikweli.
IMG_8732Mwandishi wetu aliyeshuhudia tukio hilo kinaga ubaga aliendelea kuwafuatilia wawili hao kwa kupiga picha ambazo zilidhihirisha wazi kuwa hawakuwa wao bali yale ‘maji’ waliyokunywa.
MASTAA WALIOHUDHURIA
Kwenye sherehe hiyo ambayo waalikwa walikula na kunywa, mastaa wengi walihudhuria akiwemo Mtangazaji Millard Ayo, Said Chigunda ‘Chegge’ (Bongo Fleva), Baby Madaha (Bongo Fleva), Isabela Mpanda (Bongo Fleva), Skyner Ally ‘Skaina’ (Bongo Movies) na wengineo.