Home » » TAARIFA YA IKULU KUHUSU KIFO CHA WAZIRI WA FEDHA WILLIAM MGIMWA

TAARIFA YA IKULU KUHUSU KIFO CHA WAZIRI WA FEDHA WILLIAM MGIMWA


Rais Jakaya Kikwete amepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha Waziri huyu wa fedha William Mgimwa na kwamba taifa limempoteza katika kipindi ambacho linamuhitaji zaidi kutokana na mchango wake mkubwa.

Katibu mkuu kiongozi balozi Ombeni Sefue ambae ndio ametangaza kifo cha Waziri huyu kwa niaba ya Raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, amesema Mgimwa amefariki saa tano na dakika 20 asubuhi hospitalini Afrika Kusini.

Maandalizi ya kuurudisha nyumbani mwili wa Marehemu yanafanywa na Serikali kwa kushirikiana na familia na kwamba taarifa zaidi zitazidi kutolewa kadri zitakavyopatikana
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
 
Copyright © 2011. PERUZI HABARI - All Rights Reserved
Proudly powered by Peruzitz