Hii
ni kutoka kwa majirani zetu ambapo tunaambiwa Wananchi wa Kenya wameshangazwa na
taarifa ya kuzinduka kwa mwanaume mmoja aliyedhaniwa kuwa amekufa ambapo
alizinduka akiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali moja mjini
Naivasha umbali wa kilomita tisini kutoka mji mkuu wa Kenya Nairobi.
Jamaa
huyo anaitwa Paul Mburu ana umri wa miaka 24 ambapo alipelekwa hospitalini kwa
matibabu baada ya kunywa sumu kwa lengo la kujitoa uhai kutokana na ugomvi wa
kifamilia na babake ingawa ilisemekana jamaa alifariki Jumatano usiku wakati
akipokea matibabu.
Wafanyakazi wa hospitali hiyo walipigwa na butwaa na
wengine kukimbia walipoona mwili wa mtu aliyedhaniwa kufariki ukitembea na
kuonyesha dalili za kuwa hai katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Afisa mkuu
wa matibabu katika hospitali hiyo ya wilaya Dokta Joseph Mburu amesema kuwa dawa
iliyotumiwa kumtibu Mburu hufanya moyo kupiga polepole hali ambayo huenda
ilimfanya muuguzi kudhani kuwa mgonjwa alikua amefariki.
Raia huyo wa Kenya
alisikika akimtaka mmoja wa wafanyakazi katika chumba cha kuhifadhia maiti
kumsaidia kwani alikuwa anahisi baridi kali na hapo ndipo mmoja wa wafanyakazi
alipotimua mbio kwa hofu.
Ndugu wa jamaa huyo akiwemo babake walikuwa
wametembelea chumba cha kuhifadhia maiti siku ya Alhamisi ili kuanza kwa
taratibu za mazishi lakini baadaye mchana walifahamishwa kuwa Mburu alikuwa
hai.
Mgonjwa anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya
Naivasha.
Stori ni ya bbcswahili.com
JAMAA MMOJA AFUFUKA AKIWA CHUMBA CHA KUIFADHIA MAITI
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website