Home » » MENINA AFUNGUKA "SIWEZI KUTOA RUSHWA YA NGONO ILI NITOKE KISANII"

MENINA AFUNGUKA "SIWEZI KUTOA RUSHWA YA NGONO ILI NITOKE KISANII"

MWANAMUZIKI aliyeibukia kwenye Shindano la Epiq Bongo Star Search 2012, Menina Atick amesema licha ya kusikia kuwepo kwa baadhi ya wanaume wenye nafasi kwenye ‘game’ la muziki ambao huomba rushwa ya ngono kwa wasanii wa kike ili wawatoe, yeye atakomaa na anaamini atasimama.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Menina ambaye sasa anasumbua na wimbo wake wa Shaghala Baghala alisema anachoamini ni kwamba msanii wa kike mwenye kipaji hata asipotoa rushwa ya ngono, nafasi ya kung’ara anayo, hivyo yeye atakuwa mfano kwa wengine.

“Mimi…nitoe rushwa ya ngono ili nitoke, mh…kwa kweli hiyo haiwezekani, najiamini na sitakubali kuutumia mwili wangu kwa kugawa penzi ili nisimame kwenye muziki, kwanza nitatembea na wangapi,” alihoji msanii huyo.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
 
Copyright © 2011. PERUZI HABARI - All Rights Reserved
Proudly powered by Peruzitz