Kuna
picha zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha mwanamke
akifanya mapenzi na mpenzi wake. Yote hayo yalitokea siku chache tu
baada ya mwanamke huyo kufunga ndoa na mwanaume mwingine jijini Dar es
Salaam.
Mwanamke
huyo amedai kuwa picha hizo alijipiga na mpenzi wake zamani miaka saba
iliyopita wakiwa chuoni na zimekuja kusambaa ndani ya wiki baada ya
kufunga ndoa. Anadai kuwa ni kisasi cha ex wake aliyedhamiria kuivunja
ndoa yake.
Akiongea
kwenye Ripoti ya Siku ya kipindi cha Ubaoni cha EFM kilichoruka Ijumaa
iliyopita, mwanamke huyo amedai kuwa picha hizo zimedhamlilisha mno
kiasi cha kuiharibu ndoa yake, kuwaumiza ndugu zake na kuwakosea heshima
wakwe zake na kwamba anajuta kupita kiasi.
“Ni
kweli ni mimi ndiye niliyepiga hizo picha lakini ni muda mrefu tangu
kipindi nikiwa chuo, yaani hata huyo mtu mwenyewe sijui yuko wapi sina
mawasiliano naye tena, sikutegemea kiukweli,” anasema mwanamke huyo.
“Ni
kitu ambacho kinaniuma na kimeniharibia mlolongo mzima wa maisha yangu,
mpaka sasa hivi sielewi, mume wangu hawezi kunielewa tena na yeye ndio
nimemwekea kama nguzo, ndio kila kitu kwasababu hata familia yangu
hainielewi ,” ameongeza.
“Mpaka sasa hivi sijui nafanya nini.”
Kwa upande wa mume wake, alidai kuwa picha hizo zimeuvunja moyo wake.
“Tulikuwa
tumeshaenda kwenye honey moon tumerudi, sikuamini macho yangu baada ya
kuona hizo picha na huyu mwanamke, rafiki zangu walikuwepo wengi sana,
best man wangu pia ni vitu ambavyo kuvizungumza mimi nashindwa, naanzia
wapi, lakini mapenzi huwa yako hivyo, inawezekana iko hivyo lakini sasa
kama mazingira kama yale hata kama ukiwa ni wewe lazima utaumia, familia
yangu ntaiambia nini mimi, imenigharamia harusi kubwa,” alisema mwanaume huyo.
Amedai kuwa haoni kama inawezekana tena kukaa chini na mke wake huyo kwa kile kilichotokea.
“Nikae
chini ili iweje?” alihoji kwa jazba. “Imeniuma, imeniumiza sana hii
kitu haki ya Mungu, hata kama miaka kumi imepita kwanini imekuja kwenye
harusi yangu, zawadi zimekuja kwaajili ya harusi yetu kwanini aletewe
picha za aina hiyo? Angeniambia before kwamba nilikuwa na moja mbili,
ningekuwa najua, lakini amenificha. Imenicost kwa kiasi kikubwa sana,
nitaiambiaje familia yangu kwa mfano? Nitasema nini.”
“Sitokuja kupenda tena mwanamke wa aina yoyote ile, mpaka nakuja kuingia kaburini, I swear to God, imetosha kabisa.”
Wawili hao walifunga ndoa tarehe April 23 mwaka huu.
Kwa
mujibu wa best man wa harusi hiyo, waliziona picha hizo siku nne baada
ya harusi wakati wanafungua zawadi walizopewa na kuzikuta zikiwa kwenye
bahasha na kusababisha vita kubwa kwenye familia yao.
Anadai
kuwa rafiki yake hataki kusikia chochote kuhusiana na kumsamehe mke
wake na jitihada za ndugu kuwasuluhisha zimegonga mwamba.
“Yaani hapo alipo nakuambia haelewi, mtu anayenisikiliza ni mimi tu, hasikilizi mtu yeyote. Huyo mwanamke ndio analia muda wote, jamaa haelewi,” amesema best man huyo aliyejitambulisha kwa jina la Geofrey Nicholas.
“Yaani hapo alipo nakuambia haelewi, mtu anayenisikiliza ni mimi tu, hasikilizi mtu yeyote. Huyo mwanamke ndio analia muda wote, jamaa haelewi,” amesema best man huyo aliyejitambulisha kwa jina la Geofrey Nicholas.
Sikiliza mkasa mzima hapo chini :