Kwa mujibu wa habari iliyoandiwa na gazeti la Mwanahalisi Jumanne hii,
Tale anatakiwa alipe kiasi hicho kikubwa cha fedha kwa kudaiwa kuvunja
mkataba kati yake na Sheikh Mbonde wa kuuza na kusambaza nakala za
mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya sheikh huyo.
Tale na kaka yake Idd waliamriwa na mahakama hiyo kulipa kiasi hicho
Februari 18 mwaka huu huku hati ya kukamatwa kwao ilitolewa July 8.
Mahakama ilitoa maelekezo kwa kamanda wa polisi kanda ya Ilala kuwa hadi
Jumanne hii, July 19 wawili hao wawe wamekamatwa na kupandishwa
kizimbani kujitetea kwanini wasipewe adhabu kwa kukiuka amri ya
mahakama.
Hati nyingine ilitolewa Jumanne hii kwaajili ya kukamatwa kwa Babutale.
Bongo5 imezungumza na Tale ambaye amedai kuwa makubaliano hayo
yalifanywa baina ya sheikh huyo na marehemu kaka yake, Abdu Bonge na
kwamba yeye hahusiki.
“Mimi na marehemu brother yangu tulifungua kampuni ya Tip Top Connection
pamoja, mimi nifanye muziki yeye anisaidie.. Alipoona nimesogea akaona
aachane na mimi ili afanye movie. Kwahiyo hakuwa anajua mimi
ninachokifanya kwenye muziki, mimi pia sikuwa najua anachokifanya kwenye
movie, imeenda akawa anafanya movie, sijawahi hata kushiriki hata kwa
njia ya kuonekana location, hata kukaa nao kuongea nao lolote au
kusainisha nao mkataba, so I know nothing,” amesema Tale.
“Mwaka juzi wakati nipo Uingereza yule Mzee akasikika kwenye U Heard
kwamba anaidai Tip Top Connection milioni 50. Soudy Brown alimhoji
akamuambia unamjua Babutale, akasema namjua lakini sijawahi kuongea naye
hata siku moja. Akapeleka kesi mahakamani wakati brother yupo hai
baadaye akaja akawa amefariki mimi nikawa sijui tena kinachoendelea.
Kumbe yule mwanasheria alikuwa na marehemu brother na yule mzee
wanakutana mahakamani. Mwaka huu kama mwezi mmoja uliopita akanipigia
mtu simu, simu yangu napigiwa na watu wengi sana hii ‘mimi mwanasheria,
unashtakiwa kwa kosa la kumdhulumu mtu kazi.’ Nikamuambia hizi kazi
alikuwa akisimamia marehemu brother yangu kwahiyo story unazoniletea
mimi unanirusha roho. Nikamwambia mimi naishi maisha yangu sijui
kinachoendelea na sijawahi kujihusisha na chochote na hata huyo sheikh
kama ana sehemu yoyote ambayo ameona kuna jina langu nimesaini naye niko
tayari hata akisema ananidai,” anasisitiza.
“Kwahiyo wakati wanazunguka na kesi yao wakapita Brela kuchunguza hii
kampuni wako nani na nani? Wakagundua kuna marehemu Abdul Bonge, mimi
hapa na brother yangu mwingine lakini hawajui labda kwamba sisi
tuligawana kila mtu na majukumu yake kwasababu kila mmoja alikuwa
anafanya kile ambacho anakiweza.”
“Kwahiyo wameenda mahakamani wamepata barua wanikamate kwasababu mimi
ninadaiwa. Mimi niko nyumbani wamekuja kugonga nyumbani kwangu kama
majambazi. I was like wewe unakuja unajua hapa kwa nani? Mbona unataka
kuniharrass rafiki yangu? Wewe unakuja kumkamata mtu usiyemfahamu! ‘Wewe
si Tale’ walikuwa hawajui kama mimi ndio Babutale. Kama wao wananitaka
wangeniambia mimi nipo Oysterbay polisi hapa, hawajaja. Mimi asubuhi
ndio nikatoka nikaenda kumfuaya yule mwanasheria ambaye anasimamia kesi
kuaniambia kuna nini naona kama watu wananitumia meseji kwamba
nimeshtakiwa, akanihadithia in and out.”
“Tangu nijue kila kitu leo nina siku ya nne, I know nothing, sijawahi
kumuona huyo mzee hata akitokezea sehemu simjui kwa sura. Lakini sasa
yule mwanasheria wa yule mzee anasema Babutale ana hela, tukimshtaki
Babutale atauza nyumba au watu watamchukua au tukimdhalilisha kwenye
mitandao ataona aibu atataka kulipa. Vaa kiatu changu, wewe ni sehemu
gani unalipa hapo? Sijui chochote, lakini wao wanaamini kwasababu
mahakama imewaamuru nimewalipe milioni 250 na wanaamini mimi nina hela
basi nitawalipa tu, haiwezekani,” amesema Tale.
Hata hivyo meneja huyo bado yupo njia panda kutafuta njia ya kujinasua kutoka kwenye hukumu hiyo nzito.
“Sijajua nini nitakachofanya, I know nothing,” anasema. “Anachokifanya
ameamua kunichafua bila sababu, hajui kwamba mimi najianda kuwa waziri
wa hii nchi na kuwa mbunge, anajiandaa kunifanya nionekane tapeli halafu
ni mtu wa dini labda.”
Marehemu Abdul Bonge aliyefariki March 2015 na Mbonde waliingia
makubaliano hayo June 16, 2013 kufanya biashara ya kurekodi mawaidha na
kutengeneza nakala DVDs na kuziuza nchini.
Pia alimuahidi kumjengea nyumba, kumnunulia gari na kuitangaza kazi yake
na kumpa shilingi milioni mbili na kumnunulia kanzu na kofia
(baraghashia) na kurekodi DVDs zenye ujumbe Uzito wa Kifo, Fitina Juu ya
Wanawake, Umuhimu wa Swala, Mwanadamu Yumo Ndani ya Hasara na Maadui wa
Uislam, kwa mujibu wa Mwanahalisi.
Kwa mujibu wa Jaji Augustine Jangwa, makubaliano ya awali yalikuwa
kurekodi halafu baadaye wakubaliane kuhusu bei na jinsi ya kuziuza na
kwamba badala yake waliziuza na kuzisambaza nakala hizo na kujipatia
faida bila kumshirikisha Mbonde ambaye alitumia ujuzi wake.
Awali Mbonde kupitia wakili wake Muhingo, Gwamaka Mwaikugile na Clement
Kihoko alitaka alipwe shilingi milioni 700 kama fidia ya kuvunja
makubaliano yao.
Credit: Habari hii imetumia sehemu ya habari iliyoandikwa na Mwanahalisi Online
Home »
KITAIFA
,
UDAKU
» Babu Tale Afunguka Baada ya Taarifa Kuzagaa Kuwa Kuna Amri ya Kukamatwa na Kumlipa Sheikh Milioni 250
Babu Tale Afunguka Baada ya Taarifa Kuzagaa Kuwa Kuna Amri ya Kukamatwa na Kumlipa Sheikh Milioni 250
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website