Miezi
 michache baada ya wanandoa Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ na Gardner 
Gabriel Fikirini Habash kutalikiana kwenye Mahakama ya Mwanzo Manzese 
Sinza jijini Dar, mwanaume huyo amemuanika ‘mtu wake’ wa sasa a.ka. 
‘mwendokasi’ akisema ndiye mrithi wa mikoba ya mwimbaji huyo nyota wa 
Muziki wa Kizazi Kipya.
Katika
 Viwanja vya Escape One, Kawe, jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita, 
ambako mwimbaji mahiri wa Muziki wa Dansi Bongo, Christian Bella alikuwa
 akifanya shoo ya kutimiza miaka 10 katika ‘game’, Gardner alionekana na
 mrembo huyo akizunguka naye kimahaba kutoka eneo moja kwenda lingine 
huku wadau wake wakihoji ni nani!
Garder
 alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi alikiri kuwa ni kweli kwa sasa 
anamiliki kifaa kipya kinachokwenda kwa jina la Vestina.
“Yes!
 Ndiye huyo kaka. Huyo ndiye mtu wangu kwa sasa na kama nilivyowahi 
kukudokeza, nimekuwa naye kwa muda mrefu kidogo, lakini sikuweza 
kumwanika mapema kwa sababu zinazoeleweka au ninazozijua mwenyewe,” 
alisema Gardner.
Mwandishi: “Vipi kuhusu Jide sasa, ndiyo n’tolee moja kwa moja kwa sababu ya talaka?”
Gardner: “Jide kitu gani bwana? Huyo ndo’ mwendokasi wangu kwa sasa.”
Gardner alimtaja binti huyo aliyekataa kusema umri wake kuwa anaitwa Vestina Jax, mkazi wa jijini Dar es Salaam.
Mwandishi
 wa habari hizi alilitaka kufahamu kama kuna mipango yoyote ya kufunga 
ndoa katika siku za karibuni baina yake na mrembo huyo, lakini Gardner 
alikataa kusema lolote juu ya hilo.
“Duu!
 Acha basi kaka! Kwa hilo sina comment,” alisema mtangazaji huyo ingawa 
habari za ndani zaidi zinasema kuwa, mrembo huyo ndiye mkewe mratajiwa.
Gardner: Jide Kitu Gani Bana!, Huyu Ndiye Mwendokasi Wangu Kwa Sasa
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan 
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
