Kwa nyakati tofauti, chanzo kinasema majirani waliwahi kupanda juu ya uzio wa nyumba hiyo na kutaka kupunguzwa kwa sauti ya muziki, lakini Diamond na madansa wake wamekuwa wakikaidi kwa madai kuwa hiyo ni sehemu ya kazi yao, jambo lililosababisha kuwasiliana na mmiliki wa nyumba hiyo ili amtoe msanii huyo, vinginevyo watamshtaki.
“Jamaa baada ya kuitwa na mwenye nyumba na kuambiwa kuhusu jambo hilo na kutakiwa kuhama, aliongea naye kutaka amuuzie kabisa nyumba hiyo lakini akakataa na hata alipong’ang’ania, Diamond alitajiwa bei isiyofanana hata kidogo na nyumba hiyo, akaondoka usiku-usiku kama ilivyokuwa kwa Wema kukwepa aibu,” kilisema chanzo chetu.
Jengo iliyopo Studio hiyo |