Mhubiri maarufu duniani TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations nchini Nigeria ametua jijini Dar es salaam leo tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.
Mara tu baada ya kutua uwanja wa Ndeghe wa Kimataifa wa Julius Nyerere, TB Joshua alikwenda Ikulu moja kwa moja kumsalimia Rais Jakaya Mrisho Kikwete kumsabahi na kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa uhuru na amani, huku akiondoka madarakani akiwa mtu mwenye furaha. TB Joshua amepongeza Rais Kikwete pia kwa kupata Dkt Magufuli kama mrithi wake, akimtaja Rais huyo mpya mteule kama Rais wa Tanzania wa Baraka na Fanaka tele katika awamu hii mpya.
Home »
KIMATAIFA
,
SIASA
,
UDAKU
» Mhubiri Maarufu Duniani TB Joshua Atua Tanzania, Apokelewa na Rais Kikwete Ikulu ...
Mhubiri Maarufu Duniani TB Joshua Atua Tanzania, Apokelewa na Rais Kikwete Ikulu ...
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

