Msanii huyo ametua nchini kwa tiketi ya MTV kupitia taasisi yake inayojishughulisha na kampeni za kupambana na Ukwimwi (Staying AliveFoundation) ya nchini Marekani, Kelly akiwa balozi wake.
Akiwa Uwanja wa Fisi, ambako kunasifika kwa ufuska wa kupindukia na rate kubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wasichana wadogo, Kelly alitembelea NGO ya EYG (Elizabeth Youth Group) inayojishughulisha na kutoa misaada ya elimu ya HIV/AIDS, uchangudoa, ulevi pamoja na uvutaji bangi kwa vijana nchini.