Afisa Mtendaji Mkuu na Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa Azam TV. Pichani akifanya mahojiano na Mtangazaji wa Azam TV Wasiwasi Mwambulambo
Baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV kitengo cha Huduma kwa Wateja wakiwa wameshikilia Ving’amuzi vya Azam TV wakati wa uzinduzi huo
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba (MB) katika tete-a-tete na Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd. Rhys Torrington mara baada ya kuzindua Azam TV itakayoanza kurusha matangazo yake hewani Desemba 6 mwaka huu.
Yusuf Bakhresa akizungumza jambo na watoto wake kwenye uzinduzi huo
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Bw. Boniface Wambura (kushoto) akifuatilia yanayojiri kwenye uzinduzi huo
Yusuf Bakhresa akibadilishana mawazo na wadau wa michezo nchini waliohudhuria uzinduzi huo.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba (MB) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Azam TV mara baada ya kuzindua rasmi kwenye sherehe zilizofanyika mwishoni mwa Juma Hyatt Regency The Kilimanjaro Hotel.