“Najumuika na Watanzania leo ,siku ya Ukimwi duniani ambayo hufanyika kila mwaka, kwa kuangalia wangapi wamepoteza maisha, pamoja na kuwahamasisha zaidi vijana Wakitanzania kutumia kinga ili kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi ambavyo vinapoteza nguvu ya Taifa,” alisema Lulu.
Pia Lulu alisema amekuwa akipima Ukimwi mara kwa mara ili kuangalia afya yake,huku akiwashauri vijana kwenda kupima ili kujua afya zao.
“Nimekuwa nikipima HIV kila mara katika hatua za maisha yangu,kuangalia kuhakikisha najiweka katika usalama wa afya yangu,pamoja na kupanga matarajio ya maisha.Sio kuwa ukipima ukagundulikana una HIV utashindwa kupanga malengo yako hapana! ukipata ushauri nasaha, ukajua uishi vipi kwa kuboresha afya yako, maisha yataendelea kama kawaida. Kwahiyo kinachotakiwa vijana ni kujua afya zetu mapema”