Home » , » BABY MADAHA,, ANUSURIKA KUBAKWA NA MACHOKORAA

BABY MADAHA,, ANUSURIKA KUBAKWA NA MACHOKORAA

STAA wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ amenusurika kubakwa na vijana wa kihuni nchini Kenya maarufu kama machokoraa.

Tukio hilo lilitokea  pande za Mombasa nchini Kenya wakati nyota huyo alipokuwa akirekodi video ya wimbo wake uitwao The Gal Bladder ambapo vijana hao walikatisha shughuli nzima na kuanza kumkimbiza Baby Madaha.

“Daah! Ilikuwa noma, ilikuwa usiku sasa wakati meneja wangu akinielekeza matakwa ya video hiyo ambayo yalihitaji vijana wa mtaani, ghafla wakatokea vijana wenyewe wa mtaani na kutaka kunibaka. Bahati nzuri nilifanikiwa kutimua mbio na kuwazidi,” alisema Baby.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
 
Copyright © 2011. PERUZI HABARI - All Rights Reserved
Proudly powered by Peruzitz